Font Size
Luka 22:58-62
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Luka 22:58-62
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
58 Muda mfupi baadaye, mtu mwingine akamwona Petro na akasema, “Wewe pia ni mmoja wa lile kundi!”
Lakini Petro akasema, “Wewe, mimi si mmoja wao!”
59 Baada ya kama saa moja baadaye, mtu mwingine akasema, “Ni kweli, nina uhakika mtu huyu alikuwa pamoja naye, kwa sababu yeye pia anatoka Galilaya.”
60 Lakini Petro akasema, “Wewe, wala sijui unazungumza kuhusu nini!”
Alipokuwa bado anazungumza, jogoo aliwika. 61 Bwana aligeuka akamtazama Petro kwenye macho yake. Kisha Petro akakumbuka Bwana alivyokuwa amesema ya kwamba, “Kabla ya jogoo kuwika asubuhi, utakuwa umenikana mara tatu.” 62 Kisha Petro akatoka nje na kulia kwa uchungu.
Read full chapter
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Copyright © 2017 by Bible League International